Header ads

Header ads
» » ARSENAL WATUA ARGENTINA KUKAMILISHA USAJILI WA 'MESSI'


KIONGOZI wa Arsenal, Dick Law amesafiri kwenda Argentina kukamilisha usajili wa kinda Maxi Romero.
Mkuu wa mijadala ya klabu hiyo, amepaa hadi Amerika Kusini kumalizia mpango wa kumsajili mshambuliaji kinda wa miaka 16, ambaye tayari ameanza kufananishwa na Lionel Messi.
The Gunners wamepiga hatua katika mazungumzo na Velez Sarsfield juu ya usajili wa Pauni Milioni 4.5 wa kinda huyo.

Arsenal ipo karibu kumsajili kinda wa miaka 16, Maxi Romero kutoka Velez Sarsfield kwa Pauni 4.5




Lakini dili hilo limekuwa likitiwa ugumu na haki za umilikinwa Romero- hivyo amelazimika kusafiri hadi Argentina kukamilisha mipango hiyo.
wakala wa Romero na klabu yake, Velez wote wana hisa katika kummiliki mchezaji huyo,ambayo inalketa mkanganyiko kwa Arsenal.
Ligi Kuu ya England hairuhusu mmiliki wa tatu katika sheria za usajill na suala hilo lazima limalizwe kama ya mchezaji kwenda kuanza kazi The Gunners.
Romero anatarajiwa kubaki na Velez, kwa mkopo, kwa angalau misimu miwili zaidi kabla ya kwenda England kuanza maisha mapya Arsenal. Nyota huyo kinda hajawahi kuchezea kikosi cha wakubwa cha Velez, bali amekuwa akifanya nacho mazoezi kama mchezaji wa kikosi hicho.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post