BEKI wa pembeni, Dani Alves anatazamiwa kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu baada ya mwakilishi wake kuthibitisha mlinzi huyo wa kulia wa Kibrazil amekataa ofa ya kuongeza Mkataba.
Alves amefurahia mafanikio kwa miaka saba Barcelona, akishinda mataji manne ya Hispania na mawili ya Ligi ya Mabingwa.
Lakini mkonhwe huyo mwenye umri wa miaka 31, hajawa tayari kungeza Mkataba na klabu hiyo ya Nou Camp.

Beki wa kulia wa Brazil, Dani Alves anajiandaa kuondoka Barcelona msimu huu
Wakala wa mchezaji huyo, Dinorah Santana, ambaye pia ni mke wa zamani wa Alves, amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari jana kwamba mteja wake amekataa ofa ya kuongeza Mkataba.
"Majadiliano yamekwisha," amesema mwanamama huyo.
"Ikiwa wamesema hii ni ofa ya mwisho, kisha (majadiliano yamekwisha).
Habari hizo zinatoa fursa kwa klabu ambazo zimekuwa zikimtaka beki huyo hodari kuanza kumfuatilia kuwania saini yake.
Beki huyo wa zamani wa Sevilla pia ya Hispania, amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Manchester United na Manchester City zote za England, pamoja na Paris Saint-Germain ya Ufaransa.
