Sakata la Mbunge Machachari wa Chadema, Zitto Zuberi Kabwe na chama chake cha Chadema limekuwa na visa na mikasa, vyanzo na vitendo na hatimaye leo, limefikia mwisho, limekwisha rasmi, it's over!, the rest is now a history!.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe, licha ya yeye kuwa ndio 'the most active MP of all time!', kwenye bunge la sasa, leo ameweka historia nyingine kwa kuwa ndie mbunge wa kwanza kung'atuka rasmi ubunge kwa kuaga rasmi kwa barua na kisha kulihutubia Bunge kuliaga!.
Hatua hii, sio tuu inamfanya Zitto kuendelea kuwa shujaa, bali pia kwa hatua hiyo, ameipiga Chadema bao la kisigino, kwa sababu sasa ni Zitto ndio ameiacha rasmi Chadema na sio Chadema imemfukuza!.
Uanachama wa chama cha siasa, hauombwi kwa kauli tuu bali kwa maandishi ya kujiandikisha uanachama, na kufukuzwa rasmi kwa uanachama, haufukuzwi kwa kuitishwa press conferences, kusema fulani sii mwanachama wetu, bali hufukuzwa kwa barua, hivyo mpaka hapa ninapoandika, Chadema ilimfukuza Zitto kwa kauli tuu ambayo sio kufukuza rasmi, lakini kwa barua ya Zitto, hii sasa ndio barua rasmi ya uthibitisho kuwa sasa ni Zitto ndio ameiacha rasmi Chadema!.
Ama kweli Zitto ni shujaa sijaona mfanowe!.
Hii ni threadi ya angalizo kwa Chadema na wapenzi wake, msishangilie sana hadi mkajisahau, wekeni na akiba japo kidogo ya aftermath ya kung'atuka kwa Ziito kwa sababu, kujiuzulu huku kwa Zitto, mnaweza kukuhesabu kuwa sasa ndio mwisho kabisa wa kirusi chenye jina la ZZK, and you have closed the chapter and move forward!, bora jiandaeni kabisa!, kunaweza kusiwe ndio mwisho bali sasa ndio mwanzo wa series za 'karma' effects ambazo ama zitamtandika Zitto mwenyewe kama kweli ni msaliti, ama zitaindandika Chadema, bila huruma, kama ni kweli Chadema haikumtendea haki!.
Kwa mnaoijua 'karma', shangilieni kwa kiasi tuu!, msimbeze, msimdhihaki wala msimtukane kwa sababu hakuna mkamilifu. Zitto alikuwa mwanachama wenu, hakuwabeza, hakuwatukana amewaaga rasmi kwa heshma, nanyi mnategemewa mtairudisha heshma vile vile!.
Nashauri wale msio jua "karma" ni nini, jipeni homework kidogo tuu, kisha ndio mje kuchangia!.
Nitazijibu hoja zote za msingi, ila kwa wale vichwa maji na madebe matupu, mtanisamehe, nitawashukuru tuu kwa kuchangia uzi wangu.