Wiki Ijayo, Vanessa Mdee ataachia ngoma yake ya kwanza aliyomshirikisha msanii nje ya Tanzania.
Kwenye ngoma hiyo ‘Nobody But Me’ itakayotoka na video yake, Vanessa amemshirikisha rapper wa Afrika Kusini, K.O.
K.O ni nani?
K.O ni rapper maarufu na anayekubalika nchini humo ambaye level zake
ni sawa na AKA na Cassper Nyovest. Rapper huyo alizaliwa kwa jina la
Ntokozo Mdluli huko Soweto, Johannesburg kwa wazazi wake Thembisile
Mdluli na Jabulani Mdluli.
Akiwa bado mtoto mchanga, familia yake ilihamia kwenda Piet Retief
huko Mpumalanga ambako alikulia. Wasanii waliomvutia K.O kufanya muziki
ni pamoja na Snoop Dogg na Dr Dre na walikuwa wasanii ambao walimfanya
naye atake kuwa MC na kuota kuwa siku moja naye atakuja kuwa nguli
kwenye Hip Hop na hivyo safari yake ikaanza.
Pindi K.O ameanza kufanya muziki kama kazi alikuja kukutana na Ntukza
a Ma-E kwenye chuo kikuu ha teknolojia cha Vaal ambako alipata shahada
ya mahusiano ya jamii.
Teargas
Watatu hao walianzisha kundi lao walilolipa jina la Teargas ambalo
hadi leo limeshatoa album zilizoshinda tuzo na kukubalika ‘K’shubile
K’bovu’, ‘Wafa Wafa’, ‘Dark Or Blue’ na ‘Num8er Num8er’.
Mafanikio na umaarufu wa kundi la Teargas yalimsaidia K.O
kujitengeneza kuwa staa anayejitegemea na kwa kupitia collabo
anazofanya, zimemfanya kuwa member maarufu zaidi wa kundi hilo.
Miongoni mwa collabo alizowahi kufanya ni pamoja na ‘God’s Will’ akiwa
na AKA, ‘We Rolling’ akiwa na L-Tido na ‘Just Dream’ ukiwa ni wimbo wa
kampeni ya Hansa Pilsener akiwa pamoja na Zakes Bantwini msanii wa Big
Nuz, Mampintsha.
Mwaka 2013, K.O pamoja msanii mwenzie wa kundi la Teargas, Ma-E
walijiunga na mkongwe wa masuala ya muziki na masoko Thabiso Khati
kuanzisha label ya Cashtime Life.
Vanessa Mdee na K.O
K.O akawa msanii wa kwanza wa kampuni hiyo kwa kutoa single yake ‘Mission Statement’ iliyofanya vizuri.
March 3 mwaka jana, K.O aliachia single yake ya pili ‘Caracara’ aliyomshirikisha msanii mwingine wa Cashtime Life, Kid X.
Caracara ikaja kuwa single maarufu zaidi nchini humo kwa kutawala
mawimbi ya redio na mauzo ya mtandaoni. Ngoma hiyo ilikamata nafasi ya
kwanza kwenye chart za MTV, Trace TV, Channel O, Metro FM, YFM, 5 FM,
Ukhozi FM na stesheni zingine barani Afrika.
Album ya kwanza ya K.O iliingia sokoni tarehe 27 October 2014.
August mwaka jana K.O na AKA walikuja kukutana tena kwenye ngoma
nyingine. Ni Run Jozi iliyopo kwenye album ya AKA, Levels. Ngoma hiyo
ilifanikiwa mno kwa kushika chart karibu zote maarufu.
Kwahiyo Vanessa Mdee amefanikiwa kumweka mtu mwenye nguvu mno barani
Afrika na anayechukuliwa kuwa miongoni mwa waandishi hatari zaidi wa
mashairi si nchini Afrika Kusini peke yake.