Header ads

Header ads
» » Cannavaro, Abdul wazichapa kavukavu Taifa

NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, juzi Jumatano alijikuta akivaana na beki mwenzake wa timu moja, Juma Abdul na kurushiana makonde walipokuwa wakiingia kwenye vyumba vya kupumzika wakati wa mchezo dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa.

Mtiririko wa tukio hilo ambalo lilikuwa kama filamu, katika mechi hiyo ambayo Yanga ilishinda kwa mabao 3-1 ulianza baada straika wa JKT Ruvu, Samwel Kamuntu kufunga bao katika kipindi cha kwanza.

Waanza kuzinguana
Wakati wachezaji wakielekea vyumbani, Cannavaro alimfuata Abdul na kuanza kumlaumu kwa bao hilo la Kamuntu ndipo Abdul naye akahamaki na kujibu mashambulizi kwa kujitetea kuwa hana kosa.

Baada ya kuona majibizano hayo, kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima aliingilia mzozo huo na kuwatuliza kwa kuwa mashabiki walikuwa wakishuhudia. Wawili hao wakaachana.Wakati wakitoka vyumbani kwa ajili ya kipindi cha pili, Cannavaro alionekana akimkumbatia Abdul kuashiria kuwa wamemalizana.

Nyuma ya pazia
Chanzo cha ndani kililiambia gazeti hili kuwa kumbe baada ya kuachana mbele ya mashabiki, Cannavaro alimsubiri Abdul kwenye mlango wa kuingilia katika vyumba na kuanza kumshambulia kwa kumpiga akidai alimkosea adabu, ndipo Abdul naye akajibu kwa... kumshambulia nahodha wake
huo, dakika chache baadaye wakaamuliwa na kutulizwa.

Juma Abdul afunguka:
Alipoulizwa juu ya tukio hilo na madai ya kupigana, beki huyo wa pembeni alisema: “Kweli ulitokea mzozo baada ya yeye kunishambulia wakati tukiingia kwenye vyumba, alikuwa akinilaumu kuwa nimefungisha lakini siyo kweli. Wenzetu waliingilia na kututuliza, lakini yameisha na tumemalizana.”

Cannavaro anena:
“Unajua wakati wa mechi huwa mchezaji damu inachemka, kulitokea mvutano tu wa kawaida wa kujibizana lakini hatukupigana, tuliyamaliza tu na hakuna chochote kilichoendelea baada ya mchezo.”

kumshambulia nahodha wake huyo, dakika chache baadaye wakaamuliwa na kutulizwa.

Juma Abdul afunguka:
Alipoulizwa juu ya tukio hilo na madai ya kupigana, beki huyo wa pembeni alisema: “Kweli ulitokea mzozo baada ya yeye kunishambulia wakati tukiingia kwenye vyumba, alikuwa akinilaumu kuwa nimefungisha lakini siyo kweli. Wenzetu waliingilia na kututuliza, lakini yameisha na tumemalizana.”

Cannavaro anena:
“Unajua wakati wa mechi huwa mchezaji damu inachemka, kulitokea mvutano tu wa kawaida wa kujibizana lakini hatukupigana, tuliyamaliza tu na hakuna chochote kilichoendelea baada ya mchezo.”

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post