Mtoto
mmoja wa miaka saba ametembea hadi katika nyumba moja katika jimbo la
Kentucky nchini Marekani ili kuripoti kuanguka kwa ndege aliyoabiri.
Kulingana
na polisi ndege hiyo baadaye ilipatikana imeanguka huku watu wanne
wakiwa wamefariki katika kaunti ya Lyon yapata kilomita 50 mashariki mwa
mji wa PaducahKituo cha runinga cha NBC nchini Marekani kimesema kuwa msichana huyo alimwarifu mtu aliyemfungulia mlango kwamba wazazi wake walifariki katika ajali hiyo ya ndege.
Picha ya ndege hiyo haijatolewa na polisi hawajatoa tamko lolote kuhusu uhusiano wake na waathirwa.
Shirika linalosimamia anga za juu limesema kuwa maafisa wanaodhibiti usafiri wa ndege walipoteza mawasiliano na ndege hiyo aina ya Piper PA-34 baada ya rubani kuripoti matatizo ya mitambo.