Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amemteua Dk
Mighanda Manyahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la
Umeme nchini (Tanesco), akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali
Mstaafu Robert Mboma aliyemaliza muda wake.
Baada ya uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo amewateua wajumbe wanane watakaounda Bodi hiyo
ambao ni Kissa Kilindu, Juma Mkobya, Dk Haji Semboja, Shaaban Kayungilo,
Dk Mutesigwa Maingu, Boniface Muhegi, Felix Kibodya na Nyamajeje
Weggoro.
Akithibitisha uteuzi huo, Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava alimwambia mwandishi
wa gazeti hili kuwa uteuzi huo umefanyika na tayari wajumbe wameshaanza
kazi kama walivyopangiwa.