Kumekuwa na msisimko mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii nchini Kenya kuhusu taarifa ya msichana wa Kihindi aliyekiuka
mila na tamaduni za jamii yake na kuolewa na kijana Mwafrika.
Msichana huyu wa kihindi anaitwa Sarika Patel, na ameolewa na kijana wa kabila la Bukusu Timothy Khamala, jambo ambalo ni nadra sana kwa watu wa jamii ya kihindi. Kilichowashangaza wengi ni kwamba Sarika ametoka katika familia tajiri na kuamua kuishi maisha ya walalahoi kijijini

Kwa Sarika maisha ya umaskini ambayo Timothy anaishi sio kikwazo hata kidogo bali kwake hapo ndipo anapata raha na mapenzi ambayo anasema yamemridhisha na kumtuliza nyumbani kwa kijana Timothy.

Timothy alikuwa anafanya kazi nyumbani kwa kina Sarika kama mjakazi lakini akafutwa kazi na baba ya Sarika baada ya kupendana na msichana wake.Kwa sasa yeye ni tarishi katika ofisi hii ya jimbo.Sarika hana kazi