Siku ya jumatano wanajeshi wa Afrika ya kati walimvamia mtu mmoja ambaye walishumu kuwa mpiganaji zamani wa kundi la Seleka na kumuuawa kwa mawe mchana mkweupe, huku wananchi wakishangilia.
Ufaransa imelaani vikali kitendo hicho na kuomba adhabu kali itolewe ambayo itakuwa mfano kwa wengine. Rais wa nchi hiyo Catherine Samba Panza ameamuru kufanyika kwa uchunguzi kubaini wahusika wa tukio hilo, hatuwa ambayo imeungwa mkono na Ufaransa
Akizungumza na vyombo vya habari, muakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini jamhuri ya Afrika ya kati Bubakar Gaye, amesema tukio la kumuuwa mtu hadharani huku watu wakishangilia, ni tukio baya la kulaaniwa kwa nguvu zote na kuomba uchunguzi uanzishwe mara moja ili wahusika wahukumiwe na vyombo vya sheria.