Kesi mpya imefunguliwa
dhidi ya wazalishaji (producers) maarufu T-Pain na DJ Khaled, pamoja na
Rapper Rick Ross, Pitbull na Cash Money Records, na makampuni mengine
kadhaa ya kuchapisha na record label zenye uhusiano na producers hao.
Kesi hiyo imefunguliwa na Pul Batiste anae wakilisha bendi ya Batiste
Brothers, bendi maarufu ya jazz iliyoanzishwa mwaka 1976, New Orleans,
inawashtaki kwa kuiba mziki wa Batiste familly na kuichanganya na yakwao
bila ridhaa yao wala kuwalipa chochote.
Kesi hiyo yenye kurasa 118 imewataja hasa kwa majina T-Pain, DJ Khaled,
Pitbull, Rick Ross, Ace Hood na Cash Money kama watuhumiwa, ambao
walitoa "idadi kubwa ya nyimbo zinazokiuka mashari yao.
madai hayo yanadai kuwa wimbo maarufu kama "Blame It," na "Wurk Booty"
za T-Pain na "All I Do is Win," ya DJ Khaled walichukuliwa kutoka katika
nyimbo mbalimbali zilizoundwa na Batiste familly.
"majina kibao ya nyimbo zilizozalishwa na waliotajwa wanadai
zimetengenezwa kinyume na sheria kwa kuingiza miziki ya Family Batiste
katika miziki yao."
"Ni wazi washtakiwa wameiba beat , mashairi, melody na chords kutoka
katika nyimbo za wenye mashtaka Plaintiff," madai hayo yanadai.
"nyimbo nyingi za washtakiwa zimekuwa zikiachiwa mara nyingi katika
version nyingi na kuwa kila walichokiachia kilikuwa naukiukaji wa haki
miliki," na hivyo kudai fidia ya dola 100,000,000
Mbali na wasanii na wazalishaji, makampuni ya mbali mbali ya uchapishaji
yanayomilikiwa na washitakiwa, pamoja na record label kadhaa ikiwemo
Def Jam na RCA / Jive, zimetajwa katika kesi hiyo.
Batiste inatafuta ni kutafuta kamili uhasibu, tuzo ya uharibifu halisi,
pamoja na faida na amri ya mahakama ya kudumu ya kuzuia washitakiwa
kutoka kwa kutumia nyenzo zozote zaidi zinazokiuka bila ruhusa.
BAHTISMA BLOG CHAGUO LA WATU.