Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili ambayo ni kutotii amri halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi kutenda kosa.
Sheikh
Ponda amefikishwa mjini Morogoro na helkopta ya jeshi la polisi majira
ya saa tano asubuhi chini ya ulinzi mkali ambapo askari waliimarisha
ulinzi kwa muda wote huku kikosi cha kutuliza ghasia FFU wakiwa na
silaha mabomu na mbwa ambapo hali hiyo imesababisha kusimama kwa baadhi
ya shughuli zingine za kiofisi katika ofisi zilizopo jirani na
mahakama ya hakimu mkazi wakati kesi hiyo ikiendelea ...
Akisoma
shataka mbele ya hakimu mkazi Richard Kabate , wakili mkuu wa serikali
kanda ya Morogoro Benard Kongola amedai kuwa shekh Ponda anadaiwa
kutenda makosa hayo matatu Agosti 10 mwaka huu majira ya jioni katika
viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro.
Katika
shitaka la kwanza la shekhe Ponda anadaiwa kutotii amri halali ambapo
shitaka la pili anadaiwa kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za
dini kwa kutoa maneno kuwa serikali iliamua kupeleka jeshi Mtwara
kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua na kuwatesa
wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa Mtwara ni Waislamu.
Shitaka
la tatu linalomkabili shekh Ponda ni kushawishi na kutenda kosa ambapo
anadaiwa kuwa alitoa maneno ya ushawishi kwa kuwataka waislaam
wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani
zinaundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa CCM na serikali, na kama
kamati hizo zitajitokeza aliwaamuru wafunge milango na madirisha ya
misikiti kuwapiga.
Baada
ya kusomewa mashitaka hayo shekh Ponda anayetetewa na mawakili wasomi
Barthoromew Tarimo na Ignas Punge alikataa mashataka yote matatu na
hivyo upande wa mashitaka kupinga dhamana kwa madai kuwa shekh Ponda
anatumikia kifungo cha nje na kwamba hakutakiwa kufanya kosa, hata hivyo
anakabiliwa na makosa mengine.
Upande
wa mashitaka umedai kuwa upelelezi umekamilika na kesi hiyo itasomwa
tena Agosti 28 mwaka huu ambapo mstakiwa amerudishwa rumande kwa
helkopta jijini Dar es salaam.
BAHTISMA BLOG