Habari leo hii kutoka bungeni zinaweza kuwa ni sehem nzuri ama habari nzuri kwa wanafunzi wengu huku baadhi wakiona kama ni mizinguo..
sababu inayonifanya kusema hiki, ni pale nilipowafikiria wale waliopata division 1, hofu itakua imetanda baada ya kauli ya wabunge walioteuliwa kufatilia ishu ya kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2011 / 2012, ambapo inaonekana kabisa kurudiwa kusahihishwa upya kwa mitihani hiyo
Taarifa ya tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato cha nne imesomwa bungeni leo na Mh.Lukuvi.
Mh.Lukuvi. amesema sababu zilizosababisha wanafunzi wafeli ni upungufu wa waalimu, mazingira magumu a kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa na utaratibu mbovu wa baraza la mitihani uliotumika bila kuwashirikisha wadau wa elimu
Mh.LukuviI amesema kuwa NECTA haikufuata vigezo vya kuwafaulisha wanafunzi kwa kufuata STANDARDIZATIONS na CONTINOUS ASSESSMENTS.
Hivyo basi, matokeo hayo yamefutwa na yatasahihishwa upya