Header ads

Header ads
» » Jifunze jinsi ya kufanya ikitokea umesahau patern za simu yako



Watu wengi wamekuwa wakipata shida kwa kuweka patterns ngumu kwenye simu zao n baada ya muda kusahau na kushindwa kufungua simu zao. Jifunze jinsi ya kufanya ikitokea umesahau patern za simu yako.

 Common android pattern lock idea #1
 Njia ya kwanza inaitwa “Hard Reset” Fata hatua hizi kwa umakini
  • Zima kwanza simu yako
  • Washa ukiwa umeshikilia kitufe cha kupandishia sauti na kitufe cha kuwashia simu bila kuachia vyote viwili kwa pamoja.
  • Chagua “wipe data/factory reset” .Kisha kubaliana na chagua hilo “Confirm”
  • Ikishamalizika kwa kufanya urudisho wa kiwandani, zima simu yako na uiwashe tena kwa njia ya kawaida tu sasa.
  • Kwa kufanya hivyo utakuwa umefanikiwa kuondoa password uliyokuwa umeisahau, kama njia moja ikishindikana jaribu na nyingine.
Njia namba mbili ni kwa kutumia Account yako ya Gmail,Njia hii ni endapo uliunganisha simu yako na account yako ya Gmail na bado unakumbuka hiyo email na neno lake la siri.
  1. Fungua email yako ya Gmail .
  2. Bonyeza kitufe kime andikwa “My Account”
Myaccount_SwahiliTech
3. Chagua hapo kwenye mshale mwekundu “Sign-in & security”
forget_Password_SwahiliTech
4. Hatua hii utaona vifaa vyako vyote vilivyo unganishwa na email yako, Chagua kwenye mshale mwekundu “Review device”
sahau_neno la siri_SwahiliTech

5. Sasa utaweza chagua simu yako na kufuta password uliyo isahau.
password
6.  Chagua “Remove” kuondoa password uliyo sahau kwenye simu yako. utakuwa umefanikiwa. kama njia hii pia ikishindikana fata njia inayo fuata ili kufanikisha zoezi lako.
badili_pasiwedi

Njia ya tatu na ya mwisho katika kuondoa password uliyoisahau kwenye kifaa chako cha  Android ni kwakutumia Kopyuta. Hakikisha unaunganisha kompyuta yako na kebo ya USB.kisha fata hatua hizi.
  1. Unganisha simu na Kompyuta yako kwa kutumia waya wa USB
  2. fungu kwenye kopyuta yako START->RUN–>chapa neno  CMD
  3. Kisha copy na kupesti komand zifuatazo kwenye ukurasa wako wa CMD
Adb shell
cd/data/data/com.android.providers.settings/databases
sqlite3 settings.db
update system set value=0 where name=’lock_pattern_autolock’;
update system set value=0 where name=’lockscreen.lockedout permanently’;
.quit
hadi hapo utakuwa umefanikisha kufuta password uliyo sahau kwenye simu yako.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post