Wanafunzi wa shule za wasichana Afrika Kusini waanza mradi wa kubuni na kujenga satalaiti ya kwanza ya kibinafsi barani Afrika.
Uzinduzi wa satalaiti hiyo watarajiwa kufanyika mwishoni mwaka huu utakaofanywa na mfadhili wa mradi huo ambaye ni shirika la Maendeleo ya kiuchumi ya Meta (UMEDI).
Lengo la shirika hilo ni kuhamasisha vijana wanawake wenye umri mdogo katika kujifunza Sayansi,Teknolojia ,Uhandisi na hisabati mpango unaojulikana kimataifa kama STEM.
Mradi huo pia utawahusisha wasichana kutoka nchini Kenya ,Ghana,Namibia,Malawi na Rwanda.
Utafiti umeonyesha kuwa idadi ya wanawake katika mradi wa STEM ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya vijana wanaume.
Inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2020 asilimia 80 za kazi ulimwenguni zitahitaji sharti ya ujuzi wa kisayansi,Teknoloji ana uhandisi.
Chanzo: Trt.tr