Serikali kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya Nchi wameifanyia maboresho Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2003 na kuja ya sera mpya ya mwaka 2016 ili kuunganisha sekta muhimu za uzalishaji na viwanda katika miundombinu ya TEHAMA.
Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi wa Sera ya Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016.
Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani akiwahutubia wadau
wa TEHAMA wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano ya mwaka 2016 mjini Dodoma.
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuiwezesha Tanzania kutumia fursa
zinatokana na uwepo wa miundombinu ya TEHAMA kuingia katika uchumi wa
kati ifakapo 2025 kwa kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika sekta
mbalimbali za uzalishaji nchini.Mhe. Ngonyani aliongeza kuwa Sera hiyo ni muhimu katika kujenga jamii habari itakayowezesha nchi kufikia maarifa yatakayosaidia kwenda sanajari na mpango wa Taifa kujenga uchumi wa viwanda.
Baadhi ya wafanyakazi wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wadau wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi
wa Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016
mjini Dodoma.
Alisema kuwa Sera hiyo imejikita katika kukuza matumzi TEHAMA katika
uzalishaji ili kuongeza tija , kukuza utafiti na kuvutia uwekezaji wa
sekta binafsi katika TEHAMA kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa
kwa ujumla.Awali akiongea kabla ya uzinduzi wa Sera hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Profesa Faustin Kamuzora alisema kuwa Sera hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji wa kazi wa kila siku katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema kuwa sera hii itasiaidia kwenda sanajari ya ukuaji wa kasi wa matumzi ya mawasiliano hapa nchini.