Simu za Mkononi :
Simu zinachangia ugomvi mkubwa katika familia sasa hivi. Simu zinatumika kupanga mipango ya kiharifu na kifisadi.
Wapenzi wamekuwa wakitumia simu kupanga mipango ya udanganyifu katika mahusiano, japokuwa hii ni tabia ya mtu binafsi lakini teknolojia ya simu imerahisisha mambo haya kutokea kuleta vishawishi vikubwa.
Simu za Mkononi na Mtandao wa Intaneti.
Mtandao wa intaneti katika simu na programu za kisasa za mawasiliano zimechochea moto mawasiliano baina ya watu. Urahisi huu wa kuwasiliana unatumika vibaya sasa hivi. Unapunguza sana mawasiliano ya ana kwa ana na badala yake watu wanapendelea zaidi kuwasiliana kwa simu.
Utakuta mtu yuko na mwenza wake nyumbani lakini kila mmoja yuko bize na simu yake akiwasiliana na wengine. Mawasilino ya ndani yanadhurumiwa na simu na mitandao ya kijamii.
Niliona picha moja ya vijana kadhaa waliamua kwenda kupata vinywaji pamoja lakini walipofika sehemu ya kinywaji wakaagiza kisha kila mmoja akageukia kwenye simu yake, hakuna mazungumzo tena yaliyoendelea. Hii ni hatari kubwa inayoletwa na teknolojia za kisasa katika jamii zetu.
2. Televisheni na Video (TV)
TV inaingilia mawasiliano baina ya watu wanaotazama. Badala ya kuongea na kujadili mambo ya msingi baina yao TV inakuwa kikwazo.
Tunafanya makosa haya katika familia nyingi,mgeni akija basi atapewa rimoti za ving’amuzi vyote na deki ya video. Mazungumzo yanaishia kwenye kukaribishwa tu na watatumia muda mwingi kuangalia maisha ya watu wengine katika TV badala ya maisha yao.
Matumizi ya TV yanatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu na kupunguza muda wa kuangalia. Madhara ya TV kwa Watoto
TV kwa watoto inaelezwa kuwafanya wasijishughulishe na vitu vingine kama masomo na michezo na hivyo kudumaza akili zao na kutia uvivu miili yao. Watoto wanatakiwa kuangalia TV kwa ratiba na kwa programu maalumu tu ambazo zina maadili kwa watoto na zinazowasaidia kujifunza stadi za maisha.
3. Mitandao ya Kijamii
Nimeelezea kidogo juu ya madhara ya mitandao ya kijamii hapo juu lakini niongezee zaidi hapa. Mitandao ya kijamii inakata mawasilianio ya ana kwa ana. Watu wanapendelea zaidi kuwasiliana na watu walio mbali kuliko waliopo karibu nao. Whatsapp inaongoza katika madhara na ndiyo inayopendwa nakutumiwa na wengi.
Siku hizi ukienda katika sherehe za harusi mfano utaona katika meza nyingi watu wnashughulika na simu zaidi bila kujali tukio lililowaleta hapo. Maharusi wanabaki peke yao na MC.
Sehemu za kazi pia kumekumbwa na shida kubwa,mitandao ya kijamii katika simu inaingilia utengaji wa kazi. Na tatizo hili ni wazi litachangia kupungua kwa ufanisi na uzalishaji wa mashirika na makampuni mengi kama hakutachukuliwa hatua za haraka kudhibiti madhara ya teknolojia za kisasa.
4. Kompyuta
Matumizi ya kompyuta hasa kompyuta mpakato kunaingilia mahusiano katika familia. Kwakuwa kompyuta hizi zinabebeka kirahisi watu wamekuwa wakihamisha kazi zao toka maofisini na kupeleka nyumbani.
Badala ya kushiriki na familia kama kucheza na watoto na kuongea na mwenza,utakuta mtu yuko bize na kompyuta. Hii inampa muda mdogo sana wa kuishi na familia yake. Kuna wanaohamishia kompyuta mpaka kitandani anapolala. Hii ni hatari kubwa kwa mahusiano.
Marejeo (Refference): realbuzz.com na belfasttelegraph.co.uk