Kampuni ya Facebook na Microsoft kushirikiana katika ujenzi wa nyaya za mitandao zitakazovuka bahari ya Atlantiki na kutoa huduma za mtandao kwa wateja wa Amerika ya Kaskazini na Ulaya Kusini.
Mradi huo kutoka kampuni hizo kubwa umepangwa baada ya kuwepo kwa uongezekaji wa mahitaji ya huduma za mitandao katika kanda hizo mbili.
Mradi huo utaendeshwa kwa usaidizi wa kampuni ya mawasiliano ya Uhispania ya Telefonica.
Chanzo: microsoft.com