Huduma ya WI-FI ya bure kutolewa katika miji mikubwa nchini Kenya
Serikali ya Kenya ina mipango ya kutoa WI-FI ya bure katika miji mikubwa nchini humo.
Lengo la kuwa na mpango huo ni kukuza biashara ya mawasiliano.
Katibu mkuu wa baraza la mawaziri la habari Joe Mucheru alifahamisha kuwa serikali inapanga kununua mafurushi ya data kutoka ISPs kurahisisha mawasiliano baina ya wafanyakazi na wateja wao.
Aidha alisema kuwa wafanyibiashara wengi hufanya matangazo ya bidhaa zao,hisa na huduma zao mitandaoni hasa kupitia mitandao ya kijamii kama Twitter,Facebook na Instagram.
Katibu huyo mkuu alisema kuwa wizara ya mawasiliano ikikamilisha kufanya utafiti na athari za mradi huo kwa wafanyabiashara,serikali itakuwa tayari kufanya uzinduzi.
Chanzo: standardmedia.co.ke