kwa sasa kuna TV nyingi sana kutoka makampuni mbalimbali zenye vioo vinavyo tofautiana na zinazotumia technolojia tofauti. Hili ni swali gumu sana kwani Tecnolojia za Tv na tv zenyewe zinatofautiana sana, hivyo kukufanya mtu uchanganyikiwe pale unapotaka kununua TV.
Lakini kama unataka kujua ni TV ipi ya kununua pale unapotaka kupata TV bora na yenye picha na muonekano mzuri pamoja na sauti bora.
TeknoTaarifa tumekuletea orodha ya TV bora kwa mwaka huu wa 2016
1. Panasonic TX-65CZ952
Sifa Zake
- Screen size: 65-inches
- Tuner: Freeview HD
- Resolution: 3840 x 2160
- Panel technology: OLED
- Smart TV: Custom Panasonic
- Curved: Yes
- Dimensions: 1,448 x 913 x 311 mm
Maelezo
TV hii bei yake ni kubwa kidogo lakini kama unatafuta TV nzuri
yenye uwezo wa kupendezesha sebule yako na yenye uwezo mkubwa na picha
bora TV hii inafaa sana.
Sifa Zake
- Screen size: 75-inch
- Tuner: Freeview HD and FreeSat HD
- Resolution: 3840 x 2160
- Panel technology: LED
- Smart TV: Android TV
- Curved: No
- Dimensions: 1041 x 1929 x 322mm
Maelezo
TV hii ya Sony ni moja kati ya TV bora sana kutoka katika kampuni
ya sony TV hii inasemekana kuwa na uwezo wa Android yani Android TV, Tv
hii ni moja kati ya tv bora zilizo wahi kutengenezwa na Sony kutokana
na Ubora wa picha na Sauti. Kama wewe ni mpenzi wa Sony na unapenda
Muziki na Picha bora hii Tv ni kwaajili yako
Sifa Zake
- Screen size: 55-inch
- Tuner: Freeview HD and FreeSat HD
- Resolution: 3840 x 2160
- Panel technology: OLED
- Smart TV: webOS
- Curved: Yes
- Dimensions: 760 x 1226 x 213mm
Maelezo
TV hii ya LG ni moja kati ya tv bora sana zenye uwezo wa OLED tv
hii inaonyesha picha angavu na inafaa sana kwa kutizamia filamu zenye
uwezo wa 3D, Tv hii ni Smart Tv na nimoja kati ya tv bora za sasa.
Sifa Zake
- Screen size: 48-inch
- Tuner: Freeview HD
- Resolution: 3840 x 2160
- Panel technology: LED
- Smart TV: Tizen
- Curved: No
- Dimensions: 683 x 1087 x 278 mm
Maelezo
Samsung wamefanikiwa tena kutengeneza Tv ambayo inatumia
Technolojia ya UHD. Tv hii imetengenezwa kwaajili ya watu wanaopenda
filamu na pia bei ya Tv hii ni rahisi kidogo hivyo kufanya watu kuimudu.
Sifa Zake
- Screen size: 40-inch
- Tuner: Freeview HD
- Resolution: 3840 x 2160
- Panel technology: LED
- Smart TV: Firefox OS
- Curved: No
- Dimensions: 560 x 904 x 202 mm
Maelezo
TV hii ya Panasonic ni moja kati ya Tv za kisasa zinazo tumia OS
ya FireFox. Tv hii ni Smart Tv yenye uwezo mkubwa sana kwa wapendao
application kwenye Tv, tv hii ni bora sana na inao uwezo mkubwa sana na
kama ungependa kubadilisha Tv yako kuwa kama Computer ya kisasa TV hii
ni kwaajili yako.
6. Samsung UE32J6300
Sifa Zake
- Screen size: 32-inch
- Tuner: Freeview HD
- Resolution: 1920 x 1080
- Panel technology: LED
- Smart TV: Smart Hub
- Curved: Yes
- Dimensions: 730 x 428 x 79mm
Maelezo
TV hii ya Samsung ni Tv ambayo ni nzuri zaidi kama itakua
inatumika chumbani au hata sebule ndogo au sebule ya pili katika nyumba
yako tv hii ni HD na inauwezo mkubwa wa kuweka application nyingi japo
kuwa kuna wakati inakuwa slow kidogo.
Chanzo: neurogadget.net