Mvulana mmoja kwa jina la Jani mwenye umri wa miaka 10 azawadiwa dola 10,000 na kampuni ya mtandao wa Facebook kwa kugundua jambo katika mtandao wa Instagram ambao pia unamilikiwa na kampuni hiyo.
Kijana huyo aliweza kugundua namna ambayo anaweza kufuta maandishi ya watumiaji wa Instagram.
Kijana Jani
Jani alipogundua hilo alituma barua pepe kwa Instagram na baada ya siku mbili alijibiwa.Babake Jani alisema kuwa alifurahishwa na pia kushangazwa na ugunduzi wa mwanawe Jani .
Inasemekana Jani aligundua jinsi ya kupata dosari katika mitandao na kutatua kupitia kuangalia video nyingi Youtube.
Kama shukrani kampuni ya Facebook ambayo ilimiliki Instagram mnamo mwaka 2012 ilimtunza dola 10,000.
Chanzo: mirror.co.uk