Header ads

Header ads
» » Teknolojia Mpya ya Ngozi ya Bandia inayoficha Uzee na Makovu!



Wanasayansi waja na ngozi ya bandia inayoweza wekwa juu ya ngozi ya kawaida na kuonekana kama halisi, na huku ikiwa haiathiriwi na kulowa n.k. Kundi la wanasayansi kutoka chuo cha Harvard na M.O.T huko Marekani ndio walioweza kufanya jambo hili ambalo kwa wengi linaonekana kama vile limetoka kwenye filamu kuwa jambo la halisi, linalowezekana. Eneo la jicho la kushoto kwako, ngozi bandia imetumika wakati kulia haijatumika. Tofauti inaonekana Hadi sasa watu 170 wamefanyiwa majaribio ya kujibandika ngozi bandia hii iliyopewa jina la ‘second skin’, yaani ngozi ya pili. 

Pia katika majaribio hayo imegundulika hakuna waliogundulika kupata madhara yeyote yale ya ngozi, hili likionesha ya kwamba malighafi (material) waliyotumia hayana madhara kwa ngozi za watu hao. Ngozi hii bandia ni ‘ transparent’ , na hivyo ni vigumu kugundulika kama mtu ameweka kitu chochote juu ya ngozi yake. I naweza valiwa siku nzima bila kusababisha muwasho wowote na inaweza kuhimili jasho na mvua. Utaweza nawa n.k bila kuathiri chochote, haitotoka. Muonekano wa Second Skin – ‘ngozi bandia’, pale inapokuwa inatolewa Inasemekana matajiri wengi ambao uzeeka uchagua kufanya oparesheni za kuweka nyuso zao vizuri. Kuvuta na kupunguza ngozi ili kuzipa nyuso muonekano wa ujana. 
 
Njia hii isiyohusisha oparesheni inaonekana inaweza ikawa ndio njia bora na rahisi zaidi kufanyika. Matumizi mengine yanayoonekana yatawezekana ni pamoja na kutumia ngozi hii bandia kushikilia dawa iliyopakwa katika sehemu ya ngozi. Yaani dawa itapakwa kwenye eneo la ngozi na kisha ngozi bandia kuwekwa juu yake. Inawekwaje? Itakuwa kwenye mfumo wa ‘cream’ , yaani kama mafuta ya ngozi. Kuna mchanganyiko wa mafuto hayo, utapaka ya kwanza kisha kupaka nyingine juu yake…baada ya kukaa kwenye ngozi tuu itabadilika na kuwa ngozi ya bandia

CHANZO: Techcruch

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post