Hayo yamesemwa na Saeed Sarkar, Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Teknolojia ya Nano katika Kitengo cha Sayansi cha Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ameongeza kuwa, Iran hivi sasa inashindana na madola makubwa duniani kama vile Japan, Ujerumani na Korea Kusini katika uga wa teknolojia ya Nano. Amesema hivi sasa baada ya kufikiwa mapatano ya nyuklia na kuondolewa vikwazo, nchi nyingi zinataka kushirikiana na Iran katika uga wa Nano. Amesema hadi sasa Russia, Thailand, China na nchi kadhaa za Amerika ya Latini zimetia saini makubaliano na Iran katika uga wa teknolojia ya Nano.
Nano ni teknolojia mpya inayohusu matumizi ya vitu vidogo sana na miundo yake ambayo inapimwa kuwa kati ya nanomita 1-100.
Asili ya Nano ni nanomita ambayo ni kipimo cha sehemu ya bilioni moja ya mita. Hii inamaanisha vitu ambavyo ni vikubwa kuliko atomi na vidogo mara 1000 kuliko upana wa unywele.
Chanzo: parstoday.com