Serikali ya Kenya imetangaza mpango wa kuingiza nchini sheria ya kimataifa ya mitandao kwa ajili ya kuimarisha usalama.
Idara ya udhibiti wa mawasiliano nchini humo ilitoa maelezo hapo jana na kufahamisha mpango huo wa kuanza kutumia sheria hiyo ili kukabiliana na ukiukaji wa kanuni za matumizi ya mitandao.
Sheria ya kimataifa ya mitandao ilibuniwa mwaka 2001 mjini Budapest lakini imeweza kutumiwa na nchi chache barani Afrika.
Serikali ya Kenya ina imani kwamba sheria hiyo itasaidia kupunguza uhalifu mitandaoni na kesi za unyanyasaji miongoni mwa watumiaji wa teknolojia ya internet.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na idara ya mawasiliano, takriban watu milioni 37 nchini Kenya hutumia internet kupitia simu.
Chanzo: Trt.net