Header ads

Header ads
» » Hii ndio TOP 5 ya saa za gharama zaidi duniani .



1. BREGUET GRANDE COMPLICATION MARIE-ANTOINETTE Bei: $30.000.000
 



Amini usiamini saa hii inagharimu dola milioni $30m.Saa hii ya kipekee ilichukua miaka 34 kuundwa.Yamkini aliyeagiza saa hii itengenezwe alikuwa ni mpenzi wa malkia wa Ufaransa wakati huo bi Marie Antoinette.Yeye mwenyewe hakuwahi kuiona ama hata kuitumia saa hii kwani ilikamilishwa muda mrefu, miaka 34 baada yake kupigwa risasi na kuuawa.
Abraham-Louis Breguet alipokea agizo la kutengeneza saa hiyo mwaka wa 1782 hata hivyo aliaga dunia na ikambidi mwanaye akamilishe kazi hiyo 1827 miaka minne baada ya kifo chake.

aa hii ya dhahabu iliwavutia wengi sana wakati huo.Aidha ilikuwa imekamilika wakati huo na hata sasa bado inamshiko.Moja ya sababu inayoipa thamani kubwa ni kuwa bado inaweza kutekeleza majukumu yake kikamilifu zaidi ya karne 2 baada ya kuundwa.Saa hiyo iliibiwa mwaka wa 1900.Hata hivyo ilipatikana mwaka wa 2007.

Saa hiyo kwa hivi sasa inalindwa na makavazi ya kitaifa ya L. A. Mayer nchini Israeli.Saa hii ndiyo ghali zaidi mwaka huu 2016. 

2. CHOPARD 201- CARAT Bei: $25.000.000




Saa inayoshikilia nafasi ya pili duniani katika orodha ya saa 5 bora duniani ni saa ya Chopard 201- Carat.Saa hii yenye thamani kubwa zaidi duniani katika kitengo cha mapambo imeundwa kutokana na almasi 874 nadra zaidi duniani.Iliuzwa mwaka wa 2000 kwa thamani ya dola milioni $25.
Wakati huo bei yake iligonga vichwa vya habari kote duniani.Tofauti na saa ya kawaida , CHOPARD 201- CARAT haina umbo maalum kwani almasi imeunganishwa tu kiholela bila kuzingatia hali halisia ya matumizi yake.
Chopard ina Almasi za kipekee kadhaa
1 almasi yenye umbo la moyo na rangi ya waridi , karati 15.37. – 1 Almasi yenye umbo la moyo,na rangi ya samawati, karati 12.79. – 1Almasi yenye umbo la moyo yenye rangi ya D,Karati 11.36. – 3 Almasi zenye umbo la tunda rangi ya njano karati, 8.45 . – 26 Almasi zenye umbo la tunda rangi ya Njano Karati, 17.07 – 48 Almasi zenye umbo la mduara rangi ya njano karati, 8.81 – 260 Almasi zenye umbo la tunda rangi ya D karati 60.94 – 91 Alamsi zenye umbo la mduara rangi ya, D karati 10.29. – 443 FC Almasi za FC za rangi ya manjano karati, 4.95 

3. PATEK PHILIPPE – HENRY GRAVES Bei: $11.000.000


Saa hii ya Henry Graves ilikuwa saa iliyoweka rekodi ya kuwa ghali zaidi duniani kwa kipindi kirefu.Hata hivyo saa hii iliuzwa kwa bei ya dola milioni $9 mwaka wa 1999.Amini usiamini saa hii ilitengenezwa mwaka wa 1933 mahsusi kwa ajili ya bwenyenye mmiliki wa benki bwana Henry Graves.
Mtengenezaji wake bw Patek Philippe anasema ilimchukua miaka 5 kuikamilisha saa hiyo ya kipekee.Imejijengea sifa ya kuwa saa ya pekee duniani yenye uwezo wa kutekeleza majukumu 24 kwa wakati mmoja.Henry Graves iliundwa kutokana na dhahabu.
Dhahabu yenye ubora wa karati 18.Hadi mwaka wa 2013 hakuna saa yeyote iliyowahi kuishinda saa hiyo kwa ubora.

4. HUBLOT – BIG BANG Bei: $5.000.000


Kinyume na ile saa iliyoshikilia nafasi ya 5 yenye vipuri kutoka anga ya mbali, saa hii imeshikilia nafasi ya 4 kutokana na almasi.Ukweli ni kwamba saa hii ya kipekee imeundwa kwa alamasi.Saa hii aina ya Hublot -Big bang imeundwa kwa kuunganisha Almasi 1280 zenye ubora wa karati 3 kila moja.Ilichukua mwaka mmoja wa kukata na kutayarisha Almasi hiyo inayotisha kutengeneza saa moja ya Big Bang.
Kwa sasa najua unataka kujua iwapo saa yenye thamani hiyo ya dola milioni $5 inapata mteja.Bila shaka.Mwanamuziki wa kizazi kipya Beyonce Knowles aliinunua saa hiyo na kumzawadi mumewe Jay Z katika sherehe ya kuadhimisha miaka 43. 

 
5. LOUIS MOINET METEORIS Bei: $4.600.000

Saa hii ni ya kipekee sana.Ukiitaka sharti uwe na uwezo wa kulipa nauli ya roketi kwenda hadi kwenye mwezi ilikuchukua mawe ambayo itachongwa ilikuunda sehemu muhimu ya saa hii.Hii ni baadi ya saa nne duniani ambazo zinasehemu muhimu zinazotoka katika anga ya mbali.
Saa hii ni nadra sana hivi kwamba watengenezaji wake yaani Louis Moinet hufunga safari hadi anga ya mbali kuchukua vipuri vya saa hizi zenye nembo ya MeteorisKati ya saa hizo nne 3 ndizo zenye thamani ya juu zaidi duniani
Chanzo: forbes.com

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post