Header ads

Header ads
» » Ifahamu Intel kompyuta Stick teknolojia mpya ya kompyuta

Inawezekana labda umesha-wahi kuisikia au kuiona ila kwa faida ya wale ambao hawajawai kuiona wala kuisikia ni kwamba computer stick ni teknolojia mpya ya desktop kompyuta ambapo unaweza kubadilisha screen ya TV yako kuwa kompyuta


ikiwa TV yako inatumia port ya HDMI basi uwezekano wa kutumia kompyuta hii ni rahisi kabisa kompyuta hii ilianza kutoka mwishoni mwa mwaka juzi ambapo ilitoka kwa awamu ya kwanza ambapo watu wengi walilalamika sana kutokana na kompyuta hiyo kuwa slow sana ndipo mwanzoni mwa mwaka huu kampuni ya intel ilifanikiwa kutoa kompyuta hiyo ambayo sasa imeboreshwa zaidi.
 
Ikiwa na ukubwa wa GB32 Compute stick hii inauwezo wa kufanya kazi mbalimbali za kompyuta ya kawaida kama vile kuifadhi programu mbalimbali pamoja na mafaili ya muziki pia kompyuta hii inakupa uwezo wa kuongeza memory kwani ina sehemu ya memory card ambayo ina uwezo wa kutumia memory card mpaka ya GB120 vile vile kompyuta hii ina port mbili za flash ambazo zitakuwezesha kuongeza chochote kile ili kufanya matumizi yako kukamilika kabisa.
 Intel Compute Stick Power
Kifaa hichi cha Compute stick kinauzwa kwa dollar za kimarekani $159  hii ni kwa nchini marekani tu inawezekana kuwa bei rahisi sana kwa sehemu nyingine dunia, kujua zaidi angalia video iliyopo hapo juu ili kuelewa zaidi kuhusu kompyuta hiyo ya Compute Stick.

Chanzo: engadget.com/

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post