Header ads

Header ads
» » Ifahamu Asus ROG GT51CA Kompyuta Pekee Kwaajili ya Kucheza Game



Kwa wale wapenda game Asus Rog gt51ca  ni Kompyuta maalumu kwa game, kompyuta hiyo imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana ambapo ina saa maalumu ya kuvaa mkononi ambayo inatumia (NFC) Near-Field Communication.
 ASUS ROG GT51CA 3
Kwa kutumia kifaa hicho maalumu mtumiaji wa kompyuta hiyo ya Asus Gog GT51CA anaweza kuwasha kompyuta hiyo kwa kugusa tu saa hiyo akiwa karibu na kompyuta hiyo, pia mtumiaji anaweza kuwasha sehemu maalumu ya kuhifadhi data iliyofichwa kwenye kompyuta hiyo hayo yote yanafanyika moja kwa moja kwa kutumia saa hiyo maalumu.
 ASUS ROG GT51CA 2
Kwa upande wa sifa kompyuta hiyo inauwezo wa processor ya Intel Core i7-6700K Skylake processor ambayo ina nguvu ya 4.6GHz, pia kama ungependa kuongeza memory na graphics ya kompyuta hiyo unaweza ukaongeza mpaka GeForce GTX Titan X graphics cards pamoja na RAM mpaka GB 12 kila upande. Kwa kawaida kompyuta hiyo inayo RAM ya GB 16 ya aina ya DDR4 2133MHz memory, 2800MHz pia hard disk ya M.2 PCIe 512GB SSDs.

Chanzo: Asus.com

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post