Header ads

Header ads
» » » Kijana aliyetengeneza ATM ya kutoa huduma ya kwanza akataa zawadi ya dola 30,000

Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 14 aliyetengeneza mashine aina ya ATM ya vifaa vya kutoa huduma ya kwanza (First Aid) amekataa zawadi ya dola 30,000.
Taylor Rosenthal, kutoka Alabama alikataa zawadi hiyo ambayo ilitolewa na kampuni kubwa ya kitaifa ya afya ili kuweza kuuza mashine hiyo yake.

Hata hivyo Taylor amefahamisha kuwa ana mipango ya kuuza mashine hiyo kwa dola 5,500 kila moja.
Aidha kijana huyo pia alisema kuwa atatangaza mashine hiyo ya kutoa huduma ya kwanza aina ya ATM.
Mashine hiyo ya ATM ina vifaa vya kutoa huduma ya kwanza vipatavyo vinne kila moja.

Taylor alisema kuwa alipata wazo la kutengeneza mashine hiyo baada ya kuona kuwa watoto wengi wanataabika baada ya kupata majeraha katika michezo na wazazi kutopata vifaa vingi vya kutoa huduma ya kwanza.

Chanzo ABCNews

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post