Header ads

Header ads
» » India kusajili Ma-group ya WhatsApp | Ma-Admin kuhusishwa



Serikali ya wilaya moja nchini India, Kupwara, imetambulisha utaratibu mgumu kweli kweli kwa watumiaji wa WhatsApp katika eneo lao. Utaratibu huo utawabana ma’admin wa groups pale kosa linapotendwa katika makundi waliyoyaanzisha.
Pia wafanyakazi wa serikali wameambiwa wasijihusishe na ma’group ya habari na kwamba mfanyakazi wa serikali akigundulika anashiriki katika kuongelea sera za serikali katika magroup ya WhatsApp basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. 

 
Kama kundi likikutwa linasambaza habari za uongo basi watu watakaochukuliwa hatua ni pamoja na ma’admin wanaoruhusu habari hizo zisambae kwenye makundi yao. Sheria hii inalenga kupunguza usambaaji wa taarifa zisizo za ukweli.

Makundi yote ya WhatsApp yanatakiwa kuhakikisha yamejiandikisha kwa mkuu wa wilaya hiyo. Na moja ya hatua inayochukuliwa katika uandikishaji huo inaonekana ni kuingiza namba ya chombo cha usalama katika magroup hayo ili kurahisisha ufuatiliaji wa mazungumzo


Chanzo: India today na jessynews.com

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post