Header ads

Header ads
» » Mwana Mama Mtaalam wa Teknolojia ameacha kazi Google na kuamia Facebook



Regina Duncan aliyekuwa mtendaji mkuu wa kitengo kimoja cha uvumbuzi cha Google ameondoka na kwenda kujiunga na kitengo kama hicho Facebook, Mwana Mama huyo ambaye muda wake hapo Google umekuwa wa mafanikio makubwa anaenda kujiunga na kitengo pia cha uvumbuzi katika kampuni ya Facebook. Regina Duncan anasifiwa kwa kuwa Mvumbuzi wa Teknolojia, akiwa Google alifanikiwa kuongoza miradi mbalimbali ya kibunifu na ikafanikiwa, miradi aliyoiongoza mwana mama huyo ni pamoja na ule wa kutengeneza tatoo ya kidigitali na pia miradi miwili iliyo kuwa inatengeneza simu za kijanja. 
 Regina Google
Mwana MamaRegina Duncan 
Katika makampuni makubwa sio jambo geni kwa kuajiri wafanyakazi ambao walikuwa katika kampuni ambayo ni mpinzani wako ila ni ukweli usiofichika kwamba Google imempoteza mtu ambaye alikuwa na mafanikio katika kazi alizofanya. Facebook wamempata mtu muhimu hasa katika kipindi ambacho mtandao huu unayo miradi mingi ambayo inayohitaji kiongozi ambaye ana jicho na mtazamo wa ki bunifu kama Regina Duncan. 

Akiwa facebook ataongoza kitengo ambacho kinaitwa Biulding 8 na alipo ulizwa kuhusu kuhama Google mwana mama huyo amesema kwamba hii ni nafasi yake kufanya kile kitu alikuwa anatamani kufanya siku nyingi na anahuzunika saana kuondoka Google. kwa upande wao Google wanasema kwamba wanamtakia kila la kheri mfanyakazi wao huyo wa zamani katika majukumu yake mapya.

Chanzo: New York Today & theverge.com

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post