Header ads

Header ads
» » Kampuni ya Nike yaunda viatu vya Michezo vinavyoweza kujifunga kamba vyenyewe


Kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo nchini Marekani imeunda viatu vya spoti vyenye uwezo wa kujifungia kamba vyenyewe.
Msimamizi mkuu wa kampuni hiyo Mark Parker, alitoa maelezo kwenye mkutano wa New York na kutambulisha viatu hivyo vyenye uwezo wa kujifungia kamba.
Katika mkutano huo, viatu hivyo vilitambulishwa rasmi kupitia sampuli moja aina ya Nike HyperAdapt 1.0 iliyoundwa.
Kamba zinaweza kujifunga zenyewe kwa kubonyeza vidude maalum vilivyopachikwa kwenye viatu hivyo.
Wakati huo huo, mtumiaji pia anaweza kujichagulia mtindo wa ufungaji kamba za viatu.
Viatu hivyo vilivyoundwa kwa rangi tatu tofauti vinatarajiwa kuingia sokoni kuanzia mwezi Julai mwaka huu. Bei yake bado haijabainika.

TAZAMA VIDEO YA VIATU HIVYO

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post