Header ads

Header ads
» » » Ifahamu HP Sprout kompyuta Pekee isiyotumia kibodi wala mausi


kampuni ya HP ilitengeza kompyuta ya kitofauti zaidi kuliko  zote ambazo zimeshawahi kuingia sokoni. Nayo ni HP Sprout! Hii ni kompyuta ambayo imeenda kinyume na  muonekano wa kompyuta wa zaidi ya miaka 35 ya utengenezaji wa kompyuta. 

Sifa za Kompyuta hiyo

 Kwanza kabisa imefuta utumiaji wa kibodi (keyboard) kama tulivyozizoea. HP Sprout inakupa kajikamkeka (mat) cha kioo ambacho kina sensa za mguso (touch) hivyo kazi za kibodi na mausi zinachukuliwa na eneo hili.

Holiday Photo Overlays
 Kitu chochote utakachoandika au kuchora katika eneo hili kitakuwa pokelewa na kompyuta. Pia kupitia kamera ya 3D iliyopo kwenye eneo la juu, kompyuta itaweza kupokea picha ya kitu chochote utakachoweka katika kajimkeka hako, yaani itapiga picha ya kitu/umbo husika, na utaweza kufanyia maboresha ya kiubunifu kwenye programu za ubunifu kwenye kompyuta. 

 Ukitoa uwezo wa skana (scanner) , kompyuta hii pia inauwezo wa kutumiwa kama projekta . Sifa zote hizi ndani ya kompyuta moja inaifanya HP Sprout kuwa kompyuta ya kitofauti sana. Swali kubwa ni je kompyuta hii ni kwa ajili ya watu gani na kwa matumizi gani? 

HP walisema hilo ni swali ambalo wao hawana majibu ya moja kwa moja nalo, wanategemea watumiaji kuweza kugundua wataitumiaje, lakini hadi sasa inaonekana ni kompyuta nzuri zaidi kwa wabunifu, watoto wanaopenda masuala ya sanaa kama uchoraji n.k. Lakini pia ilikuweza kuuza ata kwa watu wanaoitaji kibodi za kawaida ukinunua HP Sprout utapata kibodi na kipanya vya ‘wireless’, yaani visivyotumia waya ili kuweza kukusaidia kutotumia kamkeka ka mguso pale inapobidi. Sifa Kuu Inakuja na Windows 8.1 Kioo inchi 20 Kioo/mkeka mguso inchi 23 Prosesa Core i7 na Gb 8 ya RAM. Kompyuta hii inauzwa kwa dola 1899 za kimarekani, iliingia rasmi sokoni Novemba 9 mwaka 2014

Tazama video hii ya HP Sprout
 


CHANZO: HP.COM
MHARIRI: Abdallahmagana.com

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post