Header ads

Header ads
» » » Smartphone ya kwanza ya bei rahisi zaidi Duniani yatengenezwa India

 
Kampuni moja ya India inatarajiwa kuzindua kile kinachojulikana kuwa simu aina ya smartphone ya bei rahisi.
Kampuni ya Ringing Bells imesema kuwa simu hiyo kwa jina Freedom 251 itagharimu Rupee 500 sawa na dola 7.3,lakini vyombo vya habari nchini India vimesema kuwa itauzwa kwa Rupee 251 pekee ambazo ni sawa na dola 3.67.
Ripoti zinasema simu hiyo ina ukubwa wa 8GB na ina kamera mbele na nyuma.
India ni soko la pili kwa ukubwa la simu na lina wateja bilioni moja wanaomiliki simu.
Freedom 251 inatarajiwa kulenga soko ambalo tayari linatawaliwa na simu za bei ya chini.
 
Hii ndio modeli yetu ya kwanza na tunafikiri kwamba inaleta mabadiliko katika soko la simu,shirika la habari la AFP,lilimnukuu msemaji wa kampuni hiyo akisema.
Kwa sasa kampuni hiyo inanunua vifaa vya kutengezea simu kutoka nje kabla ya kuviunganisha nchini India,lakini ina mpango wa kutengeza vifaa hivyo nchini India katika kipindi cha mwaka mmoja ujao,aliongezea.
Kampuni ya Ringing Bells ilianzishwa miezi michache iliopita na hivi majuzi ilizindua simu ya be rahisi ya smartphone inayotumia mtandao wa 4G inayouzwa Rupee 2,999,chombo cha habari cha Press Trust kiliarifu.

Source: India Today
 >>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post