Header ads

Header ads
» » Facebook na UN washirikiana kutoa huduma ya bure ya Internet kwa wakimbizi wa Syria

 Huduma ya bure ya Internet kwa wakimbizi wa Syria

Facebook na UN yashirikiana kutoa huduma ya bure ya Internet katika kambi za wakimbizi wa Syria

Mtandao mkubwa wa jamii wa Facebook unaarifiwa kushirikiana na UN kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kutoa huduma ya bure ya Internet katika kambi za wakimbizi wa Syria.
Mkurugenzi wa Facebook Mark Zuckerberg, alitoa maelezo katika mkutano wa baraza la UN na kutangaza mpango wao wa kutekeleza mradi huo kwa ushirikiano wa UN.
Mradi huo utawawezesha wakimbizi wa Syria kutumia huduma ya Internet bila ya malipo ambapo gharama zote zitalipwa na kampuni ya Facebook.
Kufuatia mradi huo, kambi zote za wakimbizi wa Syria zinatarajiwa kuwekwa vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya matumizi ya Internet.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post