Header ads

Header ads
» » Blackberry kurudi sokoni na simu mpya zenye muundo wa kuvutia

Ujio mpya wa simu za Blackberry

Baada ya kimya kirefu, kampuni ya Blackberry inatarajiwa kurudi tena upya kwenye soko la simu kwa toleo lake la Blackberry Priv.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na ShiftDelet.Net, kampuni hiyo imetangaza mpango wake wa kuingiza simu mpya aina ya Blackberry Priv zitakazotumia mfumo wa Android.

Mkurugenzi wa Blackberry John Chen alitoa maelezo kuhusiana na simu hizo mpya na kusema kwamba zinalenga kutimiza mahitaji ya watumiaji kikamilifu kutokana na muundo wa teknolojia ya hali ya juu.

Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Blackberry Priv zitazinduliwa rasmi mwaka 2016 ingawa tarehe kamili ya uzinduzi haikubainishwa.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post