Header ads

Header ads
» » Fahamu njia rahisi za kuongeza ufanisi wa computer yako

Computer ni kifaa chenye kuhitaji matunzo na uangalizi wa hali ya juu,kwa kuwa itakapo haribika huhitaji matengenezo ya gharama sana.Kuepukana na gharama hizi mmiliki wa kifaa hiki anahitaja kufahamu njia sahihi za kutunza kifaa chake ili kupelekea ufanisi wa kazi kwa hii computer pamoja na kudumu kwa muda mrefu.

Leo tutaangalia njia ambalo unaweza ukazifuata kwenye computer yako na zikakuletea matokeo ya haraka.Hazihitaji uwe na elimu kubwa sana ya computer bali uwe ni mtumiaji wa computer inayotumia windows.     

Tatizo tutakaloliangalia leo ni ile hali ya computer kutumia muda mrefu kuwaka,kufanya kazi taratibu,kusimama bila ya kufanya kazi (stuck) kabisa au hali zozote zisizo za kawaida ambazo wengi  wamekuwa wakipoteza pesa zao kwa kupeleka computer kwa mafundi,mara nyingi maamuzi haya yamepelekea kuleta matatizo ya kudumu kwenye computer.Tutaangalia mbinu pamoja na vifaa (tools) vinavyopatikana ndani ya computer yako vinavyoweza kukusafishia computer na kuirudisha katika ufanisi wake.

Kwa watumiaji wa windows kuna tools ambazo zinaweza kukusaidia katita matatizo madogo madogo yanayohusu utunzaji wa computer.Kuna tools ambazo unaweza ukashusha(download) na kuzitumia kama vifaa vya kusafishia computer yako


Disk cleanup    
   
        

Hii hutumika kwenye windows zote ni njia rahisi na haraka ya kusafishia kifaa cha kutunza data zako katika computer (Hard Disk).


Drive Optimizer                                                  
Ili computer yako iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi unaohitajika unahitaji disk optimizer ambayo inapatikana katika computer zinazotumia windows aina zote.

Task Manager
                                                   

Hii ni njia ya kuchunguza ufanisi wa computer katika tatizo la computer kufanya kazi taratibu kupita kiasi

File History

Tunza taarifa (data) zako kuzikinga na upotevu wa aina yoyote ule.File History na System image zinakuwezesha kutunza (Backup) taarifa.


Njia nyingine ambazo unaweza kutumia katika kuitunza computer yako ni kutumia programs za bure(Free Download) zitakazo kusaidia kusafisha na kutunza Data zako hewani(cloud storage) ni System Cleaners na Free cloud storage.

CCleaner
Cloud Storage



Google Drive(15GB) na Microsoft OneDrive(7GB), hizi ni njia rahisi za kuhifadhi Data zako hewani na kuzitumia mudfa wowote utakao zihitaji.

Kwa utangulizi tumeona njia rahisi za kutumia ili computer yako iendelee kuwa na ufanisi wa hali ya juu.

Kupitia vielekezi(link) vilivyowekwa katika kila njia utaona namna ya kutumia njia moja baada ya nyingine.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post