Header ads

Header ads
» » Instagram yaweka rekodi mpya kwa kufikisha idadi kubwa ya watumiaji

Rekodi mpya katika jukwaa la Instagram

Instagram yaweka rekodi mpya kwa kufikisha idadi kubwa ya watumiaji milioni 400

Mtandao wa jamii wa Instagram unaotumiwa sana na wapenzi wa kusambaza picha mtandaoni, umeweka rekodi mpya kwa idadi kubwa ya watumiaji.
Tangu kununuliwa na Facebook miaka minne iliyopita, Instagram imekuwa ikivutia watumiaji wengi wanaoongezeka kila uchao.
Kwa sasa Instagram imeweza kufikisha watumiaji milioni 400 ikiwa asilimia 75 ya watumiaji hao wanatoka nchi za nje mbali na Marekani.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na blog rasmi ya Instagram, iliarifiwa kwamba watumiaji wengi wameongezeka kutoka nchi za Brazil, Japan na Indonesia ambapo picha zaidi ya milioni 80 husambazwa kila siku.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post