Header ads

Header ads
» » Munyarwanda huyu awapa hifadhi wakimbizi wa Syria

Mnyarwanda Anna Dushime anayeishi ujerumani katika mji wa Berlin, anaombewa Baraka baada ya kusambaza habari kwamba anawahifadhi wakimbizi kutokana na machafuko na vita nchini mwao.
Maelfu ya wananchi wa Syria wanaendelea kukimbia nchi yao kutokana na vita pamoja na machafuko.

Ujerumani ni miongoni mwa nchi zinazopokea idadi kubwa ya wakimbizi ambapo serikali ya nchi hiyo, imekubali kutoa hifadhi ya wakimbizi laki 8 (800,000).
Miongoni mwa wajerumani hawakupenda uamuzi huo pia kuna baadhi yao hawataki wahamiaji kukanyaga kwenye ardhi ya nchi yao.
Anna Dushime mwenye umri wa miaka 27 , wengi wamempa jina la msichana mwenye roho nzuri, yeye hakutega sikio la idadi kubwa ya wajerumani ambao hawataki wakimbizi nchini mwao, ambapo alitoa hifadhi kwa familia ya Mohamed.

Dushime ni msichana anayeishi nchini Ujerumani , hana uwezo wa kutosha lakini alichukuia uamuzi wa kutoa hifadhi kwa familia ya Mohamed na mke wake Roqa na watoto wao wawili wanaotoka eneo la Aleppo nchini Syria.
Anna Dushime ni miongoni mwa walionusurika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda mwaka 1994. Akiongea na CNN, alieleza kwamba alikubali kuwapa hifadhi wasyria, baada ya kufikiria giza nchi ya Rwanda iliyopitia wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi.

Anna Dushima alipata nguvu kukumbuka jinsi yeye na familia yake walivyofurushwa nchini mwaona kuelekea nchini Uganda.
Anna Dushime akiongea na CNN akiulizwa ujasili alioutumia kuweza kuwasaidia wakimbizi wa Syria
Aliongeza kuwa : Nilikumbuka jinsi mama mzazi alivyokuwa enzi za ukimbizini tukikimbia nchi yetu ,tulikuwa watoto wadogo sana, hayo ndiyo yaliyotokea wakati nilipoona wale watoto wawili [watoto wa Mohamed]”.
Wakiwa safari walipata matatizo chungu nzima ikiwa ni pamoja na njaa na kiu.
Anna Dushime,baadae walikutana na mwanaume mwenye huruma akawapa msaada wakati walikuwa ukimbizini.
Huyu mwanaume, aliona hali ya uchovu wa safari yao, na kuwapa hifadhi pamoja na chakula baada ya safari ndefu bila kupata chakula.
Alisema : Njiani tulipokuwa tunaelekea Uganda, mwanaumw alitupa hifadhi nyumbani kwake. Ilikuwa kwa mara ya kwanza tunapata maji ya kunawa, tulilala vizuri, tulifurahi sana’’.
Dushime alipokea familia hiyo na kuishi pamoja kwenye nyumba ndogo anayokodi, baadae aliwatafutia msaada , wakapata nyumba na watoto wao sasa wameisharudi shuleni.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post