Header ads

Header ads
» » Rais Kenyatta afutilia mbali ombi la walimu la kutaka kuongezwa mishahara nchini Kenya

 Mzozo wa mishahara ya walimu nchini Kenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amefutilia mbali ombi la walimu la kutaka kuongezwa mishahara kwa kiwango cha kati ya asilimia 50 – 60 nchini.
Akitoa maelezo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mgomo wa walimu zaidi ya 280,000, Kenyatta alisisitiza kushindwa kutimiza matakwa yao kutokana bajeti isiyowiana na hali ya kiuchumi.
Kenyatta aliongezea kusema kwamba ombi la awali la walimu hao la kutaka kuongezwa mishahara kama wafanyakazi wengine wa taasisi za umma lilikuwa la haki lakini kuomba tena nyongeza zaidi itapelekea wafanyakazi wengine kuwasilisha ombi pia na kuvuruga bajeti ya malipo.
Kenyatta aliyerudi nchini usiku wa Alhamisi kutoka Italia, alibainisha kiwango cha nyongeza ya mishahara kinachoombwa na walimu kuwa ni cha juu sana na huenda kikasababisha uchumi kuzorota.
Walimu wanaoendeleza mgomo nchini Kenya wameapa kutorejea kazini hadi serikali itakapowatimizia matakwa yao.
Mgomo huo ulioanzishwa wiki jana umeathiri wanafunzi wapatao milioni 12 kutokana na kusitishwa kwa elimu katika shule milioni 10 kote nchini.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post