Header ads

Header ads
» » iPhone 6S, Apple TV na iPad Pro zatambulishwa rasmi


Kampuni kubwa ya teknolojia ya Apple imetambulisha rasmi bidhaa zake mpya katika maonyesho ya kiteknolojia yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Bill Graham mjini San Francisco.
Miongoni mwa bidhaa hizo zilizotambulishwa na Apple ni iPhone 6S, Apple TV na iPad Pro.
Mkurugenzi wa Apple Tim Cook amesema kwamba maelezo ya kiufundi ya iPad Pro na vipakatalishi yataunganishwa pamoja.
iPad Pro inayoendeshwa kwa mfumo wa A9X, ina skrini yenye upana wa sentimita 32.8, na itauzwa pamoja na kicharazio na kalamu maalum ya Apple Pencil.
iPad Pro pia inaarifiwa kuwa na uwezo mkubwa wa utendaji kazi kwa kasi ya asilimia 80 zaidi kuliko tarakilishi nyinginezo. Vile vile itatumia betri linalodumu kwa masaa 10.
Apple TV nayo imeundwa kwa teknolojia ya hali ya juu na kuwa na kuweza kutumika kwa ajili ya kucheza gemu.

Vile vile simu mpya za Apple aina ya iPhone 6S na iPhone 6S Plus pia zilivutia wapenzi wengi wa tekonolojia katika maonyesho hayo.

Simu hizo mpya zitaingia sokoni Australia, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, Hong Kong, Japan, New Zealand, Porto Rico, Singapore, Uingereza na Marekani kuanzia tarehe 25 Septemba.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post