Header ads

Header ads
» » Filamu ya ‘Game Of Thrones’ yashinda tuzo 8 za Emmy kwa ubunifu bora wa kisanii

Mafanikio ya filamu ya mwendelezo ya ‘Game Of Thrones’


Filamu ya mwendelezo maarufu duniani ya ‘Game Of Thrones’ imetia fora kwenye tuzo za Emmy Awards kwa kushinda jumla ya tuzo 8 kwa ubunifu bora wa kisanii.
Tuzo hizo zinajumuisha vitengo vya utayarishaji bora, urembeshaji bora wa mazingira na timu bora ya waigizaji.
Oroha kamili ya filamu za mwendelezo zilizoondoka na tuzo za Emmy Awards ni kama ifuatavyo;
—Mtangazaji bora wa televisheni: Jane Lynch, "Hollywood Game Night," NBC.
— Sauti bora: Hank Azaria, "The Simpsons," Fox.
— Kipindi bora kisichokuwa na mpangilio: "Deadliest Catch," Discovery Channel.
— Kipindi bora kilichokuwa na mpangilio: "Shark Tank," ABC.
— Kipindi bora cha vibonzo: "Over the Garden Wall," Cartoon Network.
— Uandishi bora wa vipindi: Louis C.K., "Louis C.K.: Live at the Comedy Store," louisck.net.
— Muziki bora wa filamu: "House of Cards," Netflix.
— Muziki bora wa vipindi vya televisheni: "Bessie," HBO.
— Utunzi bora na mashairi: "Inside Amy Schumer," Comedy Central.
— Unenguaji bora wa densi: "Dancing With the Stars," ABC; "So You Think You Can Dance," Fox.
— Uigizaji bora wa filamu za mwendelezo: "Game of Thrones," HBO.
— Uigizaji bora wa vipindi maalum: "Olive Kitteridge," HBO.
— Uigizaji bora wa vipindi vya vichekesho: "Veep," HBO.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post