Header ads

Header ads
» » Samsung yaunda tablet mpya itakayoendeshwa kwa mfumo wa Windows 10

Ujio mpya wa tablet kutoka kwa Samsung

Kampuni kubwa ya teknolojia ya Samsung kutoka Korea Kusini inapanga kurudi tena kwenye soko la tablet kwa kifaa chake kipya.
Samsung iliyowahi kufanya vyema kwa uzinduzi wa tablet za Galaxy Tab A na Tab S hapo awali, imeunda tablet mpya itakayoendeshwa kwa mfumo wa Windows 10.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyovujishwa, inaarifiwa kwamba tablet hiyo yenye nambari ya usajili ya SM-W700 tayari imeshaanza kufanyiwa majaribio.

Maelezo zaidi yanaarifu kwamba tablet 10 zimeundwa na kutumwa nchini India kwa ajili ya kufanyiwa majaribio.
Tablet hizo zinatarajiwa kutambulishwa rasmi katika siku za hivi karibuni na kuingizwa sokoni kwa bei ya dola 455 nchini Marekani.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post