Header ads

Header ads
» » WATANZANIA saba wameula baada ya kuteuliwa kwenye kamati mbalimbali CAF


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Shirikisho la Soka Tanznia (TFF), uteuzi huo ulifanyika kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF kilichokutana mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Cairo, Misri.
Uteuzi huo utadumu kwa miaka miwili 2015-2017. Walioteuliwa ni Rais wa zamani wa TFF Leodegar Tenga aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Ushauri na Vyama Wanachama.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameteuliwa kuwa Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20, huku Katibu Mkuu wa TFF akiteuliwa kuwa Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 17.
Mwingine ni Richard Sinamtwa aliyeteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Rufaa, Dk Paul Marealle -Mjumbe Kamati ya Tiba. Pia Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), Lina Kessy ameteuliwa kuwa Mjumbe ya Soka la Wanawake.
Kwa sasa Kessy ni Ofisa Michezo wa Umoja wa Afrika. Crescentius Magori aliteuliwa kuwa Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post