Header ads

Header ads
» » Wafungwa zaidi ya 28 wa Kipalestina wamegoma kula gerezani


Mgomo wa njaa wa wafungwa 148 wa Kipalestina

Idadi ya wafungwa wa Kipalestina wanaoendeleza mgomo wa njaa ili kupinga shinikizo la polisi na unyanyasaji katika magereza ya Israel imefikia 148.
Mgomo huo wa njaa ulianzishwa siku ya jumatano na wanachama 120 wa chama cha kupigania ukombozi wa Wapalestina na kuendelezwa kwa siku tano gerezani.
Baadaye wafungwa 28 zaidi wanaojumuisha wanachama 26 wa chama cha kupigania demokrasia pamoja na wanachama 2 wa Ashal walishiriki kwenye mgomo wa njaa.
Mgomo huo wa njaa unalenga kukomesha ukiukaji wa haki za kibinadamu na vitendo vinavyotekelezwa dhidi ya wafungwa wa Kipalestina kinyume na sheria katika magereza ya Israel.
Kulingana na takwimu za Wizara ya Wafungwa nchini Palestina, kuna wafungwa takriban 7,000 wa Kipalestina wanaozuiwa kwenye magereza ya Israel.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post