Baada ya Windows 10 kugundulika kuwa na matatizo ya uwiano katika baadhi ya vifaa, kampuni ya Sony imetoa tahadhari kwa watumiaji wa vifaa vyake vya VAIO kutotumia mfumo huo mpya.
Sony pamoja na kampuni nyingine kubwa za kutengeneza kompyuta, zinaarifiwa kuendelea kufanya majaribio ya matumizi ya Windows 10 kwenye vifaa vyao ili kuepuka matatizo ya utendajikazi wa programu.
Majaribio hayo yanatarajiwa kufanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja au miwili, kabla ya Windows 10 kuthibitishwa kuwa na uwiano na vifaa vya kampuni mbalimbali.