Header ads

Header ads
» » Hivi ndivyo Ndoa ya mke mwenye umri wa 61 na mume wa 23 ilivyovunjika baada ya mwaka mmoja

  
Kamagaju na Habimana katika sherehe za kutoa mahari
Rwanda :Ndoa ya bi Kamagaju Jeannette na mumewe Habimana Mohammed ilivunjika , baada tu ya mwaka mmoja harusi yao ifanyike katika jimbo la mashariki, wilayani Kayonza, kijijini Gahini .

Ndoa hii ilifahamika sana katika vyombo vya habari na vijijini, watu wakishangazwa na tofauti kati ya umri wa bwana harusi na bibi harusi.
Harusi yao kanisani ilifanyika tarehe 04 mwezi Septemba, mwaka 2014.Ilikuwa mara ya kwanza Kamagaju aolewe.
Jirani ya karibu ya familia hiyo ililiambia gazeti hili kwamba ndoa ya Kamagaju na Habimana ilivunjika , takriban miezi mitatu imepita.
Jirani huyo aliendelea kusema kwamba hivi sasa Kamagaju anaishi pekee yake, huku Habimana akijilipia kodi ya nyumba, na kwamba mara nyingi Habimana huonekana akiwa na wasichana wa umri wake.
Nyumba waliokuwa wanaishia baada ya harusi, ilikuwa ni ya Kamagaju binafsi.
Makuruki ilidokezewa kwamba sababu mmoja iliyomfanya bwana Habimana kukwepa nyumba yake, ni fedha aliyoahidiwa na mkewe baada ya kumuoa Kamagaju, lakini hakupewa ahadi yake hadi aamue kuondoka.
Kabla ya kuoana, wanandoa hawa walikuwa wakipinga maneno ya watu kwamba hawatapata mtoto, wakihakikisha kwamba Mungu aliyeweza kuwapa Ibrahim na Sara mtoto wakiwa wazee, ndiye angeongoza ndoa yao hadi na kwao muujiza mwingine ufanyike wapate mtoto.
Walikuwa wanaambia watu kuwa maneno hayawezi kubadili kitu, kwa mipango yake Mola.



Kamagaju siku ya harusi yake

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post