Header ads

Header ads
» » Mfumo mpya wazinduliwa rasmi kwa ajili ya watumiaji wa WhatsApp wenye simu za iPhone

Maboresho ya mfumo wa WhatsApp kwa watumiaji wa iPhone


Mnamo mwezi Julai, mfumo mpya wa Beta v2.12.5.16 ulitolewa kwa ajili ya watumiaji wa WhatsApp wenye simu za iPhone.
Mfumo huo umetangazwa kuzinduliwa rasmi leo kwa ajili ya kurahisisha matumizi ya WhatsApp katika simu za iPhone.
Kutokana na maboresho hayo, watumiaji wataweza kufanya mabadiliko ya sauti za vitambulishi na mawasiliano kama wanavyopendelea.
Vile vile mfumo huo pia utawawezesha watumiaji kuhifadhi kumbukumbu za ujumbe wa maongezi yao pamoja na video za WhatsApp. Isitoshe, mfumo huo pia utakuwa na uwiano na kuhakikisha matumizi ya Apple Map iliyoboreshwa na kampuni ya Apple kwa ajili ya kutumika kwenye vifaa vyake.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post