Header ads

Header ads
» » Apple nao wajipanga kuja na magari yanayojiendeha yenyewe Apple icar

 

Google tayari wamefika mbali kabisa katika teknolojia ya utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe na sasa Apple pia wamejitupa katika teknolojia hiyo hiyo.

apple-car
Uhakika mkubwa juu ya kampuni ya Apple kujiingiza kwenye suala la utengenezaji wa magari umejulikana baada ya injinia mmoja wa kampuni huyo kwenda kuomba kibali cha kutumia uwanja mmoja wenye barabara kadhaa nchini Marekani kwa ajili ya majaribio ya magari hayo.
Kampuni ya Google (kwa sasa ALPHABET) tayari imefika mbali zaidi katika teknolojia ya magari yanayojiendesha yenyewe na inaonekana Apple pia imeamua kutoachwa nyuma katika hili. Wengi wanaona teknolojia ya namna hii (magari ya kujiendesha yenyewe) itakuwa kubwa sana miaka michache baadae. Na kikubwa zaidi wote, Google na Apple, wanaamini kuna umuhimu mkubwa wa vifaa kama simu na tableti kuweza kuwasiliana moja kwa moja na gari lako. Fikiria uingie kwenye gari na uweze kutumia huduma mbali mbali za simu yako bila kushika simu hiyo.

Je magari hayo yatakuja rasmi lini? Endelea kutembelea mtandao wa TeknoKona….

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post