Mahakama hiyo ilifahamisha kuwa msanii huyo alikamatwa Jumapili baada ya kuonekana katika video hiyo katika mtandao wa YouTube.
Reda al-Fouly alionekana katika video hiyo akiwa kavalia nguo fupi na kuonekana mara kwa mara akiwa nusu kifua wazi akicheza.
Muandaaji wa video hiyo ambae alifahamika kwa jina la Wael Elsedeki pia alihukumiwa akiwa safarini.
Mwezi April msanii mwingine kwa jina la Safinaz alihukumiwa kifungo cha miezi 6 baada yakamatwa kavaa nguo zenye rangi ya bendera ya Misri.
Msanii huyo aliachiwa huru kwa dhamana.