Microsoft imetangaza kupata hasara kubwa ya fedha dola bilioni 2.1 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa 2015.
Katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2015 kilichoisha tarehe 30 mwezi Juni, Microsoft iliingiza mapato ya fedha dola bilioni 22.2. Kiwango hicho kinasemekana kupungua kwa asilimia 13 ikilinganishwa na mwaka 2014.
Kumekuwa na upungufu mkubwa wa mauzo ya OEM yaliyoshuka kwa kiwango cha asilimia 22.
Hata hivyo, Microsoft inatarajia kuongeza mapato mengi zaidi kwa mauzo ya mfumo wake mpya wa Windows 10 unaotazamiwa kuingizwa sokoni mwishoni mwa mwezi huu.