Header ads

Header ads
» » Maradona afunguliwa mashtaka na mkewe wa zamani kwa wizi wa fedha dola milioni 6

 Maradona ashtakiwa kwa madai ya wizi wa fedha

Mkongwe wa soka kutoka Argentina Diego Maradona, ameripotiwa kufunguliwa mashtaka na mkewe wa zamani Claudia Villafane kwa madai ya wizi wa fedha dola milioni 6 zilizopotea kwenye akaunti ya benki yao.
Villafane mwenye umri wa miaka 52, alijitokeza mbele ya mahakama ya Buenos Aires pamoja na bintiye Giannina, na kumfungulia mashtaka Maradona.
Maradona hakuwepo mahakamani wakati madai hayo yakitolewa, lakini alituma ujumbe kupitia kipindi kimoja cha televisheni na kusema kwamba alikuwa akitaka kurudishiwa fedha zake.
Maradona alisema, ‘‘Nilikuwa nataka fedha zangu. Sikuwahi kumshtaki mtu yeyote wakati nilipoporwa na wala siwezi kumshtaki mtu sasa. Nilichokuwa nikitaka ni fedha zangu tu. Singependa kutaja jina la mtu yeyote mahakamani lakini endapo watashindwa kunirudishia fedha zangu basi sitokuwa na budi.’’
Maradona pia aliwahusia wanawe Gianinna, Dalma, Jana na mkewe wa zamani Villafane kuwa na utulivu.
Mashtaka hayo dhidi ya Maradona yalizuka baada ya mkewe wa zamani Villafane aliyemuoa mwaka 1998 na kuachana naye mwaka 2003 kugundua upungufu wa fedha dola milioni 6 kwenye akaunti yao ya benki.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post